Sasa Chadema wawajia maungoni Wazanzibari

Someni habari hii hapa chini, halafu tujadiliane namna ambavyo Wazanzibari tunaingiwa maungoni sasa na Chadema. Wanaichukulia Zanzibar kama nini kwao? Na je, hii ni hatua ya Chadema peke yake kama Chadema au na wao wanafanya kazi ya lile kundi tunaloliita ‘anti-Maridhiano?’ Je, wanalipiza kisasi chao kwa CUF, ambao wanawachukulia kuwa ni wapinzani wao zaidi kuliko walivyo CCM, au wanataka kuwakomoa Wazanzibari?

Freeman Mbowe, Mwenyekiti wa Chadema

We`ll challenge Z`bar constitution – Chadema

By Judica Tarimo
29th November 2010

In a renewed push for constitutional reforms, Chadema yesterday outlined shortfalls in the 10th Isles Constitutional amendments, it claimed have “direct, negative and irreparable” effect on the Union between Zanzibar and Tanzania Mainland.

The opposition party made public its plan to formally present a private motion in the next Parliament session to challenge Zanzibar Constitutional amendments, which it said had grossly violated the Union Constitution and fundamental principles set up by the founders – the late Mwalimu Julius Nyerere and Abeid Amani Karume.

“Although they were made to calm down protracted political problems in the Isles, the amendments are absolutely unconstitutional…we are going to challenge them in the Parliament…the union is going in the wrong direction,” said Chadema’s Director of Law, Constitution, and Human Rights, Tundu Lissu at a news conference in Dar es Salaam during which he unveiled a draft copy of the private motion to be tabled in the coming House session.

Zanzibar constitutional amendments endorsed on August 9, this year by the House of Representatives and immediately signed by the then President of Zanzibar, Amani Abeid Karume on August 13 – paved the way for the formation of a national unity government, widely praised by the national and international community as “a strategic instrument” for halting political conflicts between the rival political parties of CCM and Civic United Front (CUF).

In recent debates, constitutional lawyers have criticised the amendments generally, but Chadema yesterday cited specific shortfalls.

“Firstly, the amendments now recognizes Zanzibar as a sovereign state within the Union…such changes contradict the Union Constitution which recognises Zanzibar as part of the Union,” said Lissu.

The amendments reduced the powers of the Union president when it comes to the question of dividing regions, districts and other areas in Tanzania, Zanzibar included.

While Article 2 (2) of the Union Constitution, gives powers to the Union president, in consultation with Isles president to divide Tanzania Zanzibar into different regions, districts, and other areas to ease implementation of government activities, the amended Zanzibar constitution, Article 2 (a) gives powers to Zanzibar president to do the same without consulting the Union president.

According to Chadema, the Isles constitutional amendments affected the functions, jurisdiction and structure of the High Courts in Tanzania. Under the Union Judiciary structure, as provided in the Union constitution, appeals of cases from Zanzibar High Court are supposed to the forwarded to the Appeal Court, the highest court in the country.

“However under the amendments, Article 24 (3), all cases related to human rights would be determined by the Zanzibar High Court; they will not be taken to the Appeal Court of Tanzania,” said Lissu.

The amendments have also changed the structure of the Zanzibar government, as recognized by the Union Constitution.

Article 105 (1) (b) of the Union Constitution recognises the post of Zanzibar Chief Minister, who is one of the members of the Zanzibar House of Representatives. With the recent Isles constitutional amendments, Article 39 deleted the post of Chief Minister and introduced two new posts-First Vice President and Second Vice-President of Zanzibar.

The amended Zanzibar constitution violated the Union constitution, as it changed Article 52 (2) which talked about security agents anti-smuggling unit (KMKM), prisons and JKU, which were recognized by the Union constitution and put the agents under roof “Idara Maalum” (Special Department).

In an exclusive interview yesterday, Harold Sungusia, a lawyer from the Legal and Human Rights Centre, said: “The Isles constitutional amendments have vested more powers to the Zanzibar president in handling Isles affairs, and reduced powers of Union president in Zanzibar…On top of that, these changes disrupted, confused and contradicted many things in the management of Union issues.”

Contacted, Minister of Constitutional Affairs and Justice, Celina Kombani, declined to comment on the existing contradictions between the Zanzibar and Union constitutions, saying: “I am not concerned with the Isles constitutional amendments…ask the Isles constitutional minister…that is my comment.”

SOURCE: THE GUARDIAN

4 thoughts on “Sasa Chadema wawajia maungoni Wazanzibari

 1. Hawa CHADEMA wanataka kuchokomoa mambo, jee wanayaweza au ndio kujitia michini tu? Jee ni watwanzi?

  Kwani huu Muungano wa sasa ndivyo hao wanaowaita wao “waasisi” ndivyo walivyoutaka uwe?

  Wakimwaga ugali, sisi tutamwaga mboga.

  Afterall sisi hatuutaki hata huo Muungano feki uliopo. Kwetu sisi haya ni mavamizi na sio Muungano.

 2. Maoni haya yafuatayo yamechotwa kutoka mtandao wa ZanziNet, Jukwaa la Wazanzibari, kama yalivyotumwa na Bwana Farouk Amour, tarehe 30 Novemba 2010 – Mohammed Khelef Ghassany

  Assalaam Alaaykum,

  Wazee Wetu, Ndugu Zetu,

  UMO JA, UHURU, UADILIFU

  Qauli ya Umoja wa Wazalendo

  Kukhusu Mbinu za CHADEMA Kupinga

  Maamuzi ya Zanzibar Kwamba “Zanzibar ni Nchi”.

  Tanganyika Wanahakikisha Kuwa Zanzibar ni Koloni lao

  Yeyote atakaejaaliwa kuisoma kwa utulivu hii (hapo chini) maqala ya CHADEMA hatashindwa kugundua kwa uchungu na khasira kabisa jinsi Tanganyika wanavyoendelea kuamini na kuthibitisha nia yao kwamba Zanzibar lazima iendelee kuwa koloni lao kwa hali yoyote ile.

  Wazanzibari Wathibitisha Kuwa “Zanzibar ni Nchi”.

  Qauli ya Mhishimiwa Waziri Mkuu wa Tanganyika, Bwana Pinda; kwamba “Zanzibar si Nchi”; ni pigo kubwa kwa Wazalendo wa Kizanzibari. Zaidi, qauli hii ilithibitisha kwamba Tanganyika juuyakuwa Zanzibar wamewapa imani yao, badala yake wao Tanganyika wamekhini amana hii na daima kupanga mbinu ovu, kufika kuifanya “Zanzibar si Nchi”. Wakati huohuo, qauli hii ya Mhishimiwa Waziri Mkuu, na khasa pale aliposisitiza kwa kusema “kwa mujibu wa katiba “Zanzibar si Nchi” Wazalendo wa Kizanzibari walitambuwa wajibu wao juu ya kushikamana kwa rahaka ili kuokowa nchi yao. Machungu haya yaliinua hisia za kizalendo na kujenga Umoja na Mshikamano madhubuti kabisa, khasa pale ulivyonadiwa na Mhishimiwa Rais Aman Abeid Aman, akiwa ni Rais wa Zanzibar wakati huo, Mwenyezi Mungu Mtukufu ampe kila kheri.

  Awamu ya Rais Aman Imefufuwa Uzalendo wa Kizanzibari

  Katika miaka ya mwisho ya awamu ya Rais Aman, Alhamdulillah; Zanzibar ilishuhudia na kushirikiana katika harakati muhimu kabisa za Kizalendo. Miongoni mwa harakati hizo ni:

  Ø Wazalendo wa Kizanzibari walisherehekea Uhuru wa Zanzibar siku ile ya Disemba Kumi – 2008 na 2009.

  Ø Baraza la Wawakilishi (Bunge la Zanzibar) kwa sauti moja walipasisha kwamba mafuta, gesi na maliasili ya Zanzibar, ni milki khaasa ya Zanzibar.

  Ø Baraza la Wawakilishi (Bunge la Zanzibar) kwa qauli moja walipasisha kwamba “Zanzibar ni Nchi”, na kusainiwa na Rais wa Zanzibar, Mhishimiwa Aman Abeid Aman kuwa ni sharia ya Nchi.

  Tanganyika Wanashindwa Kuficha Ukoloni Wao

  Katika kipindi hiki na harakati hizi za Kizalendo, Tanganyika wameshindwa kuficha dhamiri yake ovu juu ya Zanzibar, dhimiri ya kuendeleza ukoloni wake kwa kutumia mbinu ya kikoloni, mbinu ya WAGAWE ILI UWATAWALE. Katika kutekeleza mbinu zake za kudumisha mfarakano kati ya Wazanzibari, Tanganyika walileta Zanzibar “Tume ya Mzee Mwinyi” kuja kuchunguwa kwanini Wazanzibari wanasimama begakwabega katika maslaha ya nchi yao. Tume hii haikufanikiwa, kwasababu Wazalendo wa Kizanzibari, yaani Baraza la Wawakilishi (Bunge la Zanzibar) walikataa kuhojiwa mmoja mmoja, qauli yao ilikuwa, ikiwa wao kuhojiwa, basi iwe kwa wote pamoja sio mmoja mmoja; hivyo tume hii ya Mzee Mwinyi ilirejea kwao mikono mitupu.

  Tanganyika Kudharau Maamuzi ya Zanzibar

  Tanganyika hawajazowea, bali khasa si maslaha yao kuona Wazanzibari wanasimama qauli moja kwa maslaha ya Nchi yao. Kutokana na uovu wao huo, kila uwamuzi wa Zanzibar, Tanganyika wanaona lazima wauzuie kwa hali yoyote ile usitekelezeke. Miongoni mwa hayo:

  Ø Walifikia muwafaka CCM na CUF kufanya sirikali ya pamoja, Dodoma / Butiama wakatoa amri kwamba lazima ifanywe kurayamaoni kuulizwa Wazanzibari “kama wanataka kusikilizana”.

  Ø Baraza la Wawakilishi, (Bunge la Zanzibar) limepasisha na kusainiwa na Rais wa Zanzibar kuwa “mafuta, gesi na maliasili ya Zanzibar ni mali khalisi ya Zanzibar”, Tanganyika wanakuja na sauti kwamba hivyo ni kinyume na katiba, (katiba ya Tanganyika); suala hili lazima lipasishwe na Bunge la Tanganyika.

  Ø Baraza la Wawakilishi, (Bunge la Zanzibar) limepasisha “Zanziba ni Nchi” na kusainiwa na Rais wa Zanzibar. Tanganyika leo hii – CHADEMA – wanazuka na kusema ni kinyume na katiba, (katiba ya Tanganyika) na kupanga kupeleka madai yao kwenye Bunge la Tanganyika kupinga maamuzi ya Zanzibar.

  Kutokana na yote haya, Bunge la Tanganyika linazidi kudhihiri kuwa ni chombo cha kuendeleza ukoloni wa Tanganyika juu ya Zanzibar. Wazanzibari kwa hali hii ndipo wanapojiuliza, “Ni kweli huu wenyekuitwa muungano” ni kwa maslaha ya Zanzibar?

  Vyama vya Siasa Visimame Qauli Moja

  Hizi mbinu za kikoloni za Bunge la Tanganyika, kufika hii leo kujitokeza CHADEMA kusimama mstari wa mbele, dhaahiri shaahiri; katika utekelezaji wa mbinu ovu hizi, ni lazima Wazalendo wa Kizanzibari kwa umoja wetu kusimama qauli moja na Baraza letu la Wawakilishi (Bunge la Zanzibar) na kupinga kwa sauti kuu kabisa hivi Bunge la Tanganyika kuwa daima ni pingamiza juu ya maamuzi ya Zanzibar. Vyama vya siasa, CCM, CUF, Jahazi Asilia, AFP, UPDP na vyenginevyo, watambue kuwa si uzalendo hata kidogo wao kunyamaza kimya na kuwacha uovu huu unatendeka. Mi muhimu na ni wajibu wao wadhihirishe uchukivu wao juu ya huu uovu wa Bunge la Tanganyika, na khasa hizi mbinu za CHADEMA, na kulitaka Bunge la Tanganyika liwache mtindo huu wa aibu, mtindo wa kudharau na kuwa ni pingamizi juu ya maamuzi ya Zanzibar. Mtindo huu hautilii nguvu, bali unazidisha kuvunja imani juu ya huu wenyekuitwa muungano.

  CHADEMA Wasitufanye Zanzibar “Mbuzi wa Muhanga”

  Iwapo CHADEMA wanayo madai yao, au hata kama wanazo tafauti zao, au hata kama wanayo mivutano yao na Bunge lao, au hata na Sirikali yao ya Tanganyika, tafadhalini wasitufanye Zanzibar kuwa ni “mbuzi wa muhanga”. Imani yetu ni kushirikiana katika ya maslaha yetu sote. Msingi wetu ni kutoridhia kwa hali yoyote ile kubomolewa maslaha yetu, ni wajibu wetu kulinda na kuhifadhi maslaha yetu kwa hali yoyote ile.

  Shukrani Zetu Kwa Rais Aman

  Kwa munasaba huu, Umoja wa Wazalendo unachukuwa fursa hii kueleza tena, shukrani zake za dhati kwa Rais Aman kwa juhudi zake za kujenga umoja na mshikamano. Vilevile shukrani zetu za dhati kwake yeye khaasa na kwa Wawakilishi wetu kwa khatuwa hii kubwa na ya kihistoria kupitisha sharia kuirejeshea Zanzibar hadhi yake kuwa ni Dola Kaamili kama vile ilivyokuwa pale ilipopata uhuru wake na kujiunga na Umoja wa Mataifa, Disemba 1963, na kuwa “Zanzibar ni Nchi”. Ni juu yetu kushikamana na kuhakikisha inaendelea kuwa “Zanzibar ni Nchi, kwa hali yoyote ile haitarajea tena vile kuwa “Zanzibar si Nchi”.

  Tunamuomba Mwenyezi Mungu Mtukufu, Subhaanahu wa Ta’aala atujaalie kila kheri na baraka na awajaalie viongozi wetu uwongozi wa kheri, uadilifu na baraka na siha na tawfiiq katika kila khatuwa za matengenezo ya nchi yetu, Aamyn.

  Wa Billahi Tawfiiq

  Umoja wa Wazalendo,

  Zanzibar

  November 30, 2010

 3. Sioni ubaya wa dhamira ya CHADEMA, na wala hakuna sehemu yoyote ambapo CHADEMA wamesema hawayataki mabadiliko waliyoyafanya Wazanzibari kwaajili ya Zanzibar ila mabadiliko hayo hayaendani na katiba ya mwungano. Kinachohitajika sasa ni au kuyakataa mabadilko yaliyofanywa na Wazanzibari au kuyakubali. Na kwa vile hakuna uwezekano wa kuyakataa, basi kinachotakiwa sasa ni kuitazama katiba ya mwungano na kuifanyia mabadiliko ili iruhusu mabadiliko yaliyofanywa na Wazanzibari kwenye katiba yao yakubalike kwenye katiba ya mwungano.

  Kwanza wanachofanya CHADEMA kina faida kubwa kwa Wazanzibari kwa vile itaruhusu katiba ya mwungano kufanyiwa marekebisho ya ku – accommodate mabadiliko ya katiba ya Zanzibar. Ikibakia kama ilivyo, mtu yeyote ana uwezo wa kuipeleka serikali ya Zanzibar kwenye mahakama ya katiba kwa kukiuka makubaliano ya mwungano. Wazanzibari ni vema wakaisaidia CHADEMA kuhakikisha katiba ya Mwungano inabadilishwa na kukidhi pande zote mbili za mwungano kama kila mmoja anaona kuna haja ya kuendelea kuwa na mwungano. Maana huwezi kuwa na mwungano ambao kila mmoja anafanya anachotaka kwa wakatai anaotaka bila ya kuwa na makubaliano ya pande zote mbili.

 4. Mimi nadhani tuache hisia na ushabiki tuangaliea madhaifu yaliyojitokeza na tuyatafutie tiba. Tutajikuta tukijadili muungano kila kukicha huku maswala ya msingi kama vile elimu, miundombinu, afya, huduma bora za jamii, ulinzi na usalama, kilimo na mashirikiano na mataifa mengine kimaendeleo tumeyaweka pembeni. Suala la Muungano kama liwe ama liwepo lahitaji maridhiano baina ya Watanzania wote nao ni wabara na visiwani.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

You may use these HTML tags and attributes: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <strike> <strong>