Shafi Adam Shafi na mjukuu wake.

Ujasiri wa kujimulika katika uandishi wa Kiswahili

Mbali na Nyumbani ni riwaya iliyoandikwa kwa muundo wa tawasifu ya mwandishi maarufu wa Zanzibar, Adam Shafi anayejulikana zaidi kama Shafi Adam Shafi. Ipo haja kubwa sasa kwa waandishi kujitolea kuandika tawasifu zao au wasifu. Kitabu kimechapishwa na Longhorn (K) Limited mwaka 2012 na uhakiki huu umeandikwa na Prof. Ken Walibora.

Rais Jakaya Kikwete

Barua ya Wazi kwa Rais Kikwete

Nchi yako Mheshimiwa Rais ni mwananachama wa jumuia zote za kusimamia haki za binaadamu baada ya kutia saini na kuridhia mikataba yote katika eneo hilo, jee huku ndio kutimiza wajibu wetu? Huku ndio kujenga imani kuwa haki za binaadamu na haki za wafungwa zinalindwa?

Timu ya Zanzibar katika miaka ya '60 baada ya moja ya ushindi wao kwenye mashindano ya mpira kanda ya Afrika Mashariki.

Zanzibar, visiwa vya michezo

Nilinufaika na simulizi za babu yangu, Juma Mzee Jimba, tulipokuwa tukitembea nyumbani kwake Kwa Karagosi (Mwembetanga), tukitokea Dar es Salaam tulikokuwa tukiishi. Akinielezea historia ya magwiji wa Kriketi, gofu, kandanda (mwenyewe akiita Futboli) tangu miaka ya 1940 hadi 1960 wakiwemo kina Marehemu Ahmed Iddi Mjasiri, Shaaban Antar, Bwan Smati (Smart), Mohamed Aoud Mfaransa,  Kassim bin Mussa,  Hijja Saleh Abdulmajham na…

Salmin Awadhi Salmin, mwakilishi wa jimbo la Magomeni. Je, ni mpinzani wa Maridhiano na Umoja wa Kitaifa wa Kizanzibari?

Makada wa CCM wanaimba nyimbo mbaya

LA Salmin Awadh Salmin kuibua rai yenye sura ya kiroja, si bure, bali ana lake jambo. Kwamba atawasilisha hoja binafsi kwenye Baraza la Wawakilishi kutaka kushawishi wajumbe kuridhia utashi wake wa kuitaka Serikali ya Mapinduzi Zanzibar iitishe Kura ya Maoni kuwauliza wananchi kama wangali wanairidhia Serikali ya Umoja wa Kitaifa (SUK), ni wazi kuwa amedhamiria…